Rais Joe Biden ameingia madarakani wakati hadhi ya Marekani ulimwenguni ilifikia rekodi ya chini.
Katika nchi 60 na maeneo yaliyofanyiwa ukusanyaji wa maoni juu ya Uongozi wa Marekani na kampuni ya Gallup katika kipindi cha mwaka 2020 kuhusu urais wa Donald Trump, kiwango cha wastani utendaji wa uongozi wa Marekani kilikuwa asilimia 22.
Miezi sita ya urais wa Joe Biden, hadhi ya Marekani duniani ilirejea kwa kiwango kikubwa. Kulingana na ukusanyaji wa maoni wa Agosti uliofanywa na Gallup katika nchi 46 na maeneo, kiwango cha wastani cha kukubalika uongozi wa Marekani kilikuwa asilimia 49.
Biden alianza urais akiwa na kiwango cha chini, amesema Thomas Schwartz, mwanahistoria wa mahusiano ya nje ya Marekani katika Chuo Kikuu cha Vanderbilt.
“Nchi chache sana nje ya nchi, kwa kiwango cha juu zaidi huko Israel na Saudi Arabia, Donald Trump alikuwa akichukiwa na viongozi wengi zaidi wa kigeni na ilivyo kwa mkato kutokuwa Trump ilikuwa ni faida ya haraka,” amesema.
Hata hivyo, kutokuwa madarakani Trump kuliweza kumfikisha Biden hadi hapa, amesema Schwartz. Licha ya kurithi kutoka kwa mtangulizi wake hatma ya kuyaondoa majeshi Afghanistan, Utekelezaji uliokuwa na maafa ya kuondoka Afghanistan uliofanywa na Biden uliiharibia sana sifa ya Marekani kimataifa na hadhi yake ya kuwa inaushindani ndani ya nchi.
“Ugaidi umeongezeka, na Taliban kuchukua madaraka kumepelekea kuwekewa vikwazo vilivyoiweka Afghanistan katika hali ya mgogoro mkubwa wa kibinadamu ambao unaweza kusababisha njaa kubwa,” amesema Michael Kugelman, mshiriki wa ngazi ya juu kwa katika Kituo cha Wilson kinachoangazia eneo la Kusini mwa Asia.
“Na nafikiri kuwa huu mgogoro wa kujiondoa Marekani unaonekana unafungamana na matokeo hayo.”
Kujiondoa kuliko harakishwa kulisaliti washirika wa Magharibi na wengine, ikiwemo wanawake wasomi waliongezeka nchini Afghanistan ambao watataabika zaidi chini ya Taliban, amesema Kenneth Weinstein, mtafiti mwenye kuheshimika wa Walter P. Stern katika Taasisi ya Hudson.
Itakuwa vigumu zaidi kwa marias wa Marekani kuwataka washirika wetu kujitolea kwa malengo ya pamoja siku za usoni, ameongeza.
Weinstein alieleza kuhusu utawala ulivyoshughulikia suala la mpaka wa eneo la Kusini kama ni kufeli kwingine. Kadiri mgogoro ulivyoongezeka, Weinstein amesema, Marekani imerejea tena “kutoa maelezo yaliochakachuliwa ya sera za utawala wa Trump ambazo kampeni ya Biden-Harris ilizilaani kuwa siyo za kibinadamu mwaka 2020.