Bethlehem yasheherekea Krismas licha ya masharti ya COVID-19

Licha ya mwaka wa pili wa kuwepo kwa masharti ya kusafiri kwa sababu ya COVID -19, mji wa Bethlehem, eneo ambako alizaliwa Yesu, lilifufua sherehe zake za kila mwaka za mkesha wa Krismasi.

“Mwaka jana, sherehe zetu zilikuwa kwa njia ya mtandao, lakini mwaka huu tunaonana uso kwa uso na ushiriki na mkubwa,” Meya wa Bethlehem Anton Salman aliliambia shirika la habari la Associated Press.

Katika siku ya kawaida ya Krismani, mji wa kibiblia ni kituo maarufu sana kwa watalii kutoka kote ulimwenguni. Wastani wa watalii milioni 3 wanafika hapo kila mwaka. Umati mdogo zaidi ulihudhuria sherehe za huko Bethlehem siku ya Ijumaa, zikiambatana na hali ya hewa ambayo haikuwa nzuri. 

“Inashangaza sana,” amesema Kristel Elayyan, mwanamke wa kiholanzi ambaye ameolewa na mpalestna, ambapo alifika Bethlehem kutoka Jerusalem. “Kama ni mwaka mmoja, ni jambo la kufurahisha,” aliliambia shirika la habari la AFP. “Lakini huu ni mwaka wa pili na hatufahamu nini kitatokea siku za usoni, ni hasara kubwa sana kwa watu hapa.” 

Matukio yalijumuisha gwaride la kiasili na sherehe za mitaani. Bengi ya Skauti iliyokuwa na ngoma na bendera ilikusanyika huko Manger Square kushereheak sikukuu.

Wakati sherehe zilipunguzwa mwaka huu, Salman alikuwa na matumaini kwamba shamra shamra za mwaka 2021 zitavuka zile za mwaka jana, wakazai walipolazimika kusherehekea ndani ya nyumba zao kwasababu ya masharti ya kufunga shughuli, AP imeripoti.

Israel imepiga marufuku usafiri wote wa anga kuingia nchini humo, ambapo yalidumu kwa miaka miwili, kuendelea kuwazuia watalii kuingia katika eneo wanalokalia kimabavu la Ukingo wa Magharibi, na pia mji wa kihistoria. 

Marufuku ya kusafiri ili kuzuia kusambaa kwa Covid 19 iliondolewa Novemba li kuwaruhusu watalii wa kigeni lakini mara tu ilirejeshwa tena kutokana na kirusi omicron ambacho kimekuwa kikiambukiza kwa kasi. Sambamba na msimu wa sikukuu, kirusi kipya kimedumaza sherehe za krismasi.

Bila ya mmiminiko wa watalii, maafisa wa ndani walitumaini kwmaba jamii ndogo ya wakristo katika mji mtakatifu wataendeleza hisia za sikukuu.

Without the flood of tourists, local authorities hoped that the Holy Land’s small Christian community would keep the holiday spirit alive. 

Latin Patriarch Pierbattista Pizzaballa, kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki katika mji mtakatifu, alishiriki misa ya usiku katika kanisa la Nativity, ambako inasemekana kuwa Yesu alizaliwa. 

“Ukilaingisha na krismasi yam waka jana, ushiriki ni mkubwa saa, na hii ni dalili ya kutia moyo,” aliuambia umati wa waumini, lakini alisikitika kutokuwepo kwa waumizi wa kigeni kwasababu ya janga.

“Tunawaombea na wakati huo huo kuomba sala zao, ili yote haya yamalizike haraka na kwamba mji wa Bethlehem kwa mara nyingine tena ujae mahujaji,” amesema kwa mujibu wa AFP.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii