John Mnyika "Kikosi Kazi Kiliundwa ili Kuchelewesha Katiba Mpya"

Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuundwa kwa Kikosi Kazi ni matumizi mabaya ya Fedha za Watanzania na hivyo Serikali itoke hadharani na iseme kimetumia Fedha kiasi gani


Asema Maoni ya Wananchi kuhusu #Katiba yalikusanywa na Tume ya Warioba, hivyo hakukuwa na haja ya kuundwa kwa Kikosi Kazi zaidi ya kurudi kwenye kitabu cha Maoni ya Wananchi kilichoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba


Ripoti imetoa Mapendekezo 18 ikiwemo Kuruhusiwa Mikutano ya Kisiasa na Kuendelea Mchakato wa Katiba Mpya ingawa Rais Samia alitoa angalizo kwamba mapendekezo hayo siyo Amri kwa Serikali


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii