Waamuzi wafungiwa muda usiojulikana

CHAMA cha Soka Mkoa wa Mjini Magharib kimewasimamisha waamuzi wawili na kumfungia kutochezesha ligi mmoja kwa kushindwa kumudu Sheria 17 za soka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Mkoa huo, Ally Iddi Shaban inasema kamati yao ilikaa na kupitia ripoti za viwanjani kuanzia mzunguko wa kwanza wa ligi hadi wa nne.

Baada ya kikao hicho kamati ilitoa maamuzi ya kuwasimamisha waamuzi wawili Nurdin Mohammed Salum na Muhamed Mfupi kwa kipindi kisichojulikana kucheza mechi ndani ya mkoa huo huku Khatib Makame akifungua kuchezesha ligi ya mkoa

Mbali na adhabu hizo, pia kamati imewafungia baadhi ya wachezaji kwa kufanya vurugu uwanjani na kuhatarisha amani ya mchezo husika ambao ni Abrazak Juma (Bweleo Warriors), Fahmi Mohammed na Mohammed Khamis wa Nyangobo FC.

Pia kamati hiyo imezitoza faini ya Sh 200,000 Bweleo Warriors na Nyangobo FC, faini hizo wanatakiwa kulipa kabla ya Oktoba 21, mwaka huu.

huo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii