Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan leo Jumanne ya tarehe 18 Oktoba, 2022 amefanya ziara fupi kwenye ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Kigoma.