Yoweri Museveni "Jenerali Muhoozi Kainerugaba - atakaa mbali na mitandao ya kijamii kufuatia jumbe zake za kivita kuhusu Kenya."
Jenerali Muhoozi alitishia uhusiano wa Kenya na Uganda baada ya kusema kupitia mtandao wa Twitter kuwa anahitaji chini ya wiki mbili kushambulia na kuteka jiji la Nairobi akiwa na jeshi lake.
“Haiwezi kutuchukua wiki mbili, mimi na jeshi langu, wiki mbili kuteka Nairobi. Ninafurahi kuwa wanachama wa wilaya yetu nchini Kenya wamejibu ujumbe wangu wa Twitter. Lakini bado ni wiki mbili kwa Nairobi,” Muhoozi alisema.
Kufuatia ujumbe huo, Rais Museveni amesema kuwa mwanawe atakaa mbali na mitandao ya kijamii na kuashiria kuwa anaitumia vibaya.
"Ataondoka. Baada ya kujadili na tuliamua kuwa hawezi. Kwa sasa sababu Twitter sasa ni njia ya kisasa ya mawasiliano na ana vijana ambao anapatana nao sana. Lakini suala ni kipi ambacho tunazungumza kukihusu kwenye Twitter," Rais Museveni alisema.