Foby atoa ya mayoni juu ya Hamisa Mobeto

Msanii wa Bongofleva foby ameamua kutoa ya moyoni mwake kwa hamisa mobetto ambaye hawako sawa hivyo akihitaji wamalize tofauti zao.


Foby ametumia insta story yake kumuangukia Mobetto na kuomba yaishe kwa kile alichoeleza kuwa ame-miss kuona picha zake baada ya kulambishwa block na mrembo huyo kwa takribani miaka 3 baada ya kuwa na utofauti.


@fobyofficial ambaye bado anaeendelea kufanya vizuri na wimbo wake uitwao #Chakula uliotoka miezi miwili iliyopita aliomshirikisha Linah, inasemekana mgogoro wake na Mobetto ulianza baada ya @hamisamobetto kuachia wimbo wake wa kwanza ambao ni #MadamHero huku Foby akiwa mwandishi wa kazi hiyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii