Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi linamshikilia Elizabeth Ngiba (32), kwa kosa la kujirekodi video na kutoa lugha ya maudhi dhidi ya Wazanzibar akiwaambia kwamba licha ya kujua kujistiri lakini tabia zao ambazo hakuzitaja hazitofautiani na wengine na kuwataka wabadilike.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Elisante Mmari amesema kuwa mwanamke huyo alijirekodi video hiyo Oktoba 15, 2022, majira ya saa 8:38 mchana, na kutoa lugha hizo za maudhi dhidi ya watu wengine jambo ambalo ni kosa kisheria.
Upelelezi wa shauri hilo umekamilika na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kesho Oktoba 18, 2022, ili kujibu tuhuma zinazomkabili.