SERIKALI imezindua Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS 2022-2023) na kueleza kuwa kiwango cha maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI kimeshuka na kufikia asilimia 4.7. Pia imedhamiria kudhibiti maambukizi ya VVU kwa kuongeza uelewa kwa wananchi,kujua hali zao za maambukizi ya VVU, kujiunga na huduma za matibabu ya VVU,kuongeza uelewa na ujuzi wa kukabiliana na janga hilo nchini. Aidha utafiti uliofanywa mwaka 2016/17 ulionyesha idadi ya wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliojitambua ilikuwa 61%, waliokuwa kwenye tiba 92% na waliofikia ufubazaji VVU 87%, matokeo ambayo umuhimu wake ulisaidia kuunda mkakati wa Kitaifa wa mwitikio wa VVU na UKIMWI.