Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati akielekea Mkoa wa Kigoma leo Jumapili, Oktoba 6, 2022, Rais Samia amesema yeye na wasaidizi wake wapo kwa ajili ya kuitumikia Tanzania na Mtanzania ili kulete maendeleo.
“Tutunze amani twende tukachape kazi kila mmoja achangie maendeleo ya taifa letu, ukifanya kazi vizuri, ukiuza madini yako Serikali ikachukua kakodi ndio haya mabilioni yanayosemwa hapa yanakuja, ukienda ukilima, ukiuza mazao yako Serikali ikachukua kakodi tunazikusanya ndio maendeleo haya tunaleta.
“Sisi ni wakusanyaji wa fedha ili tulete maendeleo kwenu, hatukusanyi ili tuzibebe sisi hapana! Tunazikusanya na ndo haya mapesa mnayosikia mama amemwaga… mama amemwaga ni kwasababu tunakusanya kutoka kwenu,”amesema
Hata hivyo Rais Samia amepingana na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shakaambaye amewataka wakazi hao kuendelea kuzaa akidai Rais Samia atawajengea shule pamoja na vituo vya Afya.
“Ndugu zangu sasa mnataka nini? Zaeni tu mama yupo, madarasa yanajengwa zaeni tu mama yupo, vituo vya Afya vinajengwa, zaeni tu mama amefungua fursa wawekezaji wanakuja,”
Naye Rais Samia akajibu “Mheshimiwa hilo la zaeni tu hapana bwana, jana nimesimama Buselesele pale naambiwa kituo kimoja kinazalisha watoto 1,000 kwa mwezi. Sasa hayo madarasa baada ya miaka mitatu ni mangapi? Kama ni vituo vya Afya vingapi? Tani za chakula ni ngapi? Kwahiyo kidogo speed tupunguze kidogo,"
Awali Waziri wa Madini na Mbunge wa Bukombe, Dk Dotto Biteko amesema wakati Rais Samia anaingia madarakani kata mbili wilayani Bukombe hazikuwa na sekondari lakini baada ya mwaka mmjoa kata hizo zikakamilisha shule za sekondari.
“Na juzi mama umeleta fedha nyingi sana, ilikuwa kila tukitaka kuanzisha form one (kidato cha kwanza) kila mwaka tunafukuzana kuchangishana, sisemi kuchangishana jambo baya hapana. Nachotaka kusema mama (Rais Samia) mzigo huu ametuondolea
“Leo anafanya mwenyewe na sisi tunabaki kupeleka watoto wetu shuleni. Ametuletea fedha nyingi za kujenga madarasa 126 na mama tumekubaliana tutafungua shule za sekondari mpya nne ambazo hazikuwepo kwenye Wilaya yetu ya Bukombe,”amesema
Dk Biteko amemshukuru Rais Samia kwa kuwaruhusu wakazi wa Isodelo kukaa kwenye kijiji chao ambao awali waliitwa wavamizi pamoja na kujenga kiwanda cha asali huku akidai mwaka 2025 wakazi wa wilaya hiyo wanajua chakufanya kwakuwa kazi anazozifanya zinamtangaza.
“Mnakumbuka watu wa Idoselo toka miaka ya 80 (1980) mimi nakua, nachunga ng'ombe watu wa Idoselo wao ni wateja wa kuchapwa fimbo kila siku, wameitwa wamevamia. Wamekaa humo kama wakimbizi mama ameingia tu cha kwanza akasema hataki taharuki, watu wa Idoselo akasema kaeni na alichofanya cha ajabu kabisa amewajengea shule mpya na barabara akawafungulia,”