Tanzania yashtua Ulimwengu wa soka katika Kombe la Dunia chini ya miaka 17

Timu ya taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania (Serengeti Girls) sikua ya  Jumamosi iliushtua Ulimwengu wa soka baada ya kuifunga timu ya taifa ya Ufaransa mabao 2-1 kwenye fainali za Kombe la Dunia la FIFA nchini India.

Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru huko Margao.

Mabao ya Serengeti Girls yalifungwa na Diana Mnally kunako dakika ya 16 na Christer Bahera aliyefunga bao lapili katika dakika ya 56 kwa njia ya penati.

Ushindi dhidi ya timu ya Ufaransa unaipa matumaini timu hiyo ya Tanzania inayoshiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo kusonga mbele zaidi ya hatua ya makundi.

Ufaransa walijipatia bao la kufuta machozi kupitia kwa Lucie Calba kunako dakika ya 77 kwa njia ya penati.

Serengeti Girls ilipoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya timu kali ya Japan kwa jumla ya mabao 4-0 kwenye uwanja huo.

Nao Ufaransa katika mechi yao ya ufunguzi walitoka sare 1-1 na Canada katika mechi yao ya kwanza ya Kundi D.

Tanzania, sasa itamenyana na Canada Jumanne katika mchezo wao wa mwisho kuamua timu zitakazoingia hatua inayofuata.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii