Hamisa Mobeto " Mwanaume Anayenioa Amepata Chombo"

Hamisa Mobeto Hamisa Mobetto ambaye ni mwanamke staa nchini Tanzania anayetajwa kuwa mwenye mvuto kuliko wote kwa sasa ambaye amefunguka na kuungwa mkono kwamba, mwanaume wake amepata chombo wakati huu akiwa katika maandalizi ya ndoa yake.

Miezi kadhaa iliyopita, Hamisa alidai kupewa zawadi ya gari la kifahari aina ya Range Rover Evoque na mpenzi wake ambaye hakutaka kumuweka wazi.

Hamisa ambaye ni staa wa muziki, filamu na mitindo anasema kuwa, anajiandaa na ndoa, lakini kikubwa anachojua ni kwamba mwanaume anayemuoa atakuwa amepata chombo safi.
“Mimi ninachojua mwanaume wangu anayenioa amepata chombo,” anasema Hamisa ambaye ni mama wa watoto wawili anaowalea mwenyewe"

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii