Wachezaji 15 wa kike wajiuzulu

 wachezaji 15 wa timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania wamejiuzulu wiki chache baada ya minon'gono ya kuwepo kwa mgawanyiko kwenye kambi ya timu hiyo.

Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kwamba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wanataka kocha Jorge Vilda kuondolewa. Shirikisho la Soka la Uhispania, RFEF limechapisha taarifa jana jioni iliyosema wachezaji hao 15 waliwatumia barua pepe zinazofanana wakisema wanajiuzulu wakidai mazingira yaliyopo yanawaathiri na yasipobadilishwa hawataichezea timu hiyo.

Hata hivyo shirikisho hilo limesema litawatumia tu wachezaji wallio tayari kukitumikia kikosi hicho. Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwenye historia ya soka ya Uhispania na ulimwenguni kwa ujumla.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii