Magonjwa yasiyoambukiza husababisha asilimia 74 ya vifo duniani

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema magonjwa yasiyoambukiza kama saratani, kisukari na matatizo ya moyo yamechangia asilimia 74 ya vifo vyote duniani, na kushauri kuwa kupambana na maradhi hayo kunaweza kunusuru maisha ya mamilioni ya watu. WHO imesema magonjwa hayo yanayoepukika kwa kubadilisha mtindo wa maisha, yanauwa watu milioni 41 kila mwaka kote duniani, milioni 17 miongoni mwa hao wakiwa na umri wa chini ya miaka 70. Ripoti ya shirika hilo yenye kichwa kisemacho, ''Namba zisizoonekana'' imeonyesha kuwa magonjwa ya moyo, kisukari na saratani hivi sasa yanauwa watu wengi duniani kuliko maradhi ya kuambukiza. Aidha, ripoti hiyo imesema kinyume na imani ya wengi, magonjwa hayo sio tatizo kubwa tu katika nchi zilizoendelea, na kubainisha kuwa asilimia 86 ya vifo vya watu wenye umrri mdogo hutokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii