Tanzania na Msumbiji Zatia Saini Mikataba ya Ulinzi na Usalama

Msumbiji na Tanzania Septemba 21, 2022 zimesaini mikataba miwili ya ushirikiano mjini Maputo inayolenga kupambana na ugaidi na uhalifu.

Msumbiji kwa sasa inapambana na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo lenye utajiri wa gesi kaskazini mwa Cabo Delgado nchini humo.

 

Mikataba hiyo ilisainiwa ikiwa ni sehemu ya ziara rasmi ya siku tatu ambayo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anafanya nchini Msumbiji.Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii