Kazakhastan yaitisha uchaguzi wa mapema wa Rais

Kazakhstan imetangaza leo kuwa itafanya uchaguzi wa mapema wa rais mnamo Novemba 20 unaolenga kuufanyia ilichokiita "mageuzi makubwa" mfumo wa kisiasa wa taifa hilo la uliokuwa Muungano wa Kisovieti. Tangazo kuhusu uchaguzi huo limetolewa na tovuti rasmi ya ikulu ya nchi hiyo mapema leo Jumatano. Amri ya kuitishwa uchaguzi iliyotiwa saini na rais Kassym-Jomart Tokayev inasema uchaguzi huo utakuwa mwanzo wa safari ya kuleta uzani baina ya mihimili ya dola ikiwemo kugawanya nguvu za maamuzi kutoka kwa rais hadi kwa bunge la nchi hiyo. Tangazo hilo limetolewa wiki chache tangu serikali ya rais Tokayev kupitisha sheria ya kupunguza kipindi cha rais kukaa madarakani kuwa muhula mmoja wa miaka saba pamoja na kubadili jina la mji mkuu wa taifa hilo lililotokana na jina la mtawala wa muda mrefu wa nchi hiyo Nursultan Nazarbayev na kurudi katika jina lake la zamani la Astana.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii