Rapa cardi B " harusi yangu ni sasa"

Rapa Cardi B kutoka Marekani, ameweka wazi kuwa ni muda wa harusi yake sasa na mumewe rapa Kiari Kendrell Cephus maarufu kama Offset, baada ya kufikisha miaka mitano ya ndoa yao.


Fahamu, kwenye moja ya mahojiano ya rapa Cardi B mwaka 2019 alifunguka kuhusu harusi yake ambayo kwa mwaka huo aliahirisha kufanya, alikaririwa akisema, “Tutatumia fedha nyingi katika harusi yetu, sidhani kama ni sawa kumuacha Offset kulipa kila kitu, nahisi nitalipa zaidi yake kwani gauni langu huenda likagharimu dola 50,000.”

Cardi B na Mumewe Offset wamejaaliwa kupata watoto wawili


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii