TANZANIA YAANZA KUDHIBITI EBOLA MIPAKANI

Serikali ya Tanzania imeanza kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji katika mipaka ya nchi na viwanja vya ndege kupitia mikakati sita ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliotangazwa nchini Uganda jana usiingie nchini.

Jana Uganda ilitangaza mlipuko huo baada ya watu sita kufariki huku mgonjwa mmoja vipimo vya maabara kudhibitisha kuwa anaugua ugonjwa huo katika Wilaya ya Mubende iliyopo katikati ya nchi hiyo.


 leo Septemba 21, 2022 Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale amesema wamepitia tahadhari zote na kuamsha utayari na mifumo na ule wa majibu kwa kuangalia utayari wake wa kufanya kazi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii