Chelsea imemfuta kazi Mkurugenzi wa Biashara, Damian Willoughby mwezi mmoja baada ya kuajiriwa kutumikia nafasi hiyo. Willoughby alibainika alikuwa akituma jumbe zisizofaa na kumdhalilisha Wakala wa Fedha za Soka, Catalina Kim.
Catalina alikwenda kulalamika kwa Uongozi juu ya unyanyasaji aliofanyiwa na Willoughby kabla ya kuajiriwa ambapo uchunguzi ulifanyika kuthibitisha tuhuma hizo.