Rais Samia Awasili Msumbiji

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Maputo nchini Msumbiji kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini humo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Septemba 21, 2022 na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Rais Samia amewasili usiku wa kuamkia leo nchini humo na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Filipe Nyusi.

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Msumbiji zimekuwa na ushirikiano wa karibu katika maeneo muhimu ikiwemo ulinzi, sekta za elimu, maji, ujenzi na usafirishaji.

Rais Samia amewasili Msumbiji kwa ziara ya siku tatu akitokea Uingereza kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth II.

Kiongozi huyo mkuu wa nchi alikuwa miongoni mwa viongozi zaidi ya 200 walioshiriki mazishi hayo wakiwemo wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ambapo aliwasili London Septemba 17 na kupokewa na mwakilishi wa Mfalme Charles III, Cynthia Gresham.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii