Biden awasili Uingereza kwa mazishi ya Malkia Elizabeth 11

Rais wa Marekani Joe Biden aliwasili nchini Uingereza jana jioni kabla ya mazishi ya Malkia Elizabeth 11 siku ya Jumatatu.Haya ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. Ndege aliyosafiria Biden iliwasili katika uwanja wa ndege wa Stansted mjini London muda mfupi kabla ya saa nne usiku. Biden anatarajiwa kutoa heshima zake za mwisho katika gereza la marehemu na kukutana na mfalme mpya Charles wa 111 hii leo kabla ya mazishi ya kitaifa ya siku ya Jumatatu. Hata hivyo mkutano uliokuwa umepangwa kati yake na waziri mkuu mpya wa Uingereza Liz Truss umefutiliwa mbali. Ofisi ya waziri mkuu huyo ya Downing Street imesema, badala yake, wataanda mkutano kamili wa pande mbili wakati wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano. Hata hivyo, haikutoa maelezo zaidi kuhusu kwa nini mkutano wa awali na Biden ulifutiliwa mbali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii