Rais Joe Biden wa Marekani na wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wanatarajiwa kukutana leo hii katika Ikulu ya White House kwa mazungumzo yatakayojikita katika vita vya Urusi nchini Ukraine, maswala ya mazingira, biashara na mengineyo.Ramaphosa ni miongoni mwa viongozi wa Afrika ambao wamedumisha msimamo wa kutoegemea upande wowote baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, na Afrika Kusini ilijiepusha na kura ya Umoja wa Mataifa ya kulaani Urusi kwa uvamizi huo.Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Afrika Kusini, Naledi Pandor amesema katika mkutano wake na Biden, Ramaphosa atasisitiza haja ya mazungumzo ili kupata suluhu ya vita hivyo na kadahalika pale atakapozungumza na kwa wakati tofauti na Makamu wa Rais Kamala Harris.