Naibu wa waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amezungumza hii leo bungeni kuhusiana na kauli iliyotolewa na makamu wa rais Dkt Mpango wakati akiwa mwanza kuhusiana na na kutumia maji ya maiti kuhifadhia samaki na nyama ili zisiharibike.
"Naomba niwatoe hofu Watanzania , hakuna jambo linalohusu, tuchukue samaki kutoka Mwanza, tulete Dodoma au tupeleke Dar es Salaam, kwa kuhifadhi na maji ya maiti, halipo jambo la namna hiyo...samaki wanaovuliwa na wavuvi wetu na wanaokwenda katika masoko mbalimbali wako salama, hawana shaka yoyote". amesema Abdallah Ulega.