Kanye West Avunja Mkataba na Kampuni ya Kuuza na Kusambaza Bidhaa Zake "Nitafanya Mwenyewe"

Rappa na mfanyabiashara Kanye West 'YE' anaripotiwa kuwa amefikia maamuzi ya kuvunja mkataba wake na Kampuni Ya GAP iliyokuwa ikihusika na uuzaji pamoja na usambazaji wa bidhaa za #YEEZY.


Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wall Street Journal, Kanye West ameamua kumtuma mwanasheria wake Nicholas Gravante Jr, kuitaarifu GAP kuwa anasitisha nao mkataba wa ubia katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa zake, ikiwa ni miaka nane imesalia ya mkataba huo.

Fahamu, mkataba wa YE na GAP ulianza rasmi mwaka 2020, ambapo YE alisaini mkataba wa miaka 10 na kampuni hiyo.


Aidha, mapema wiki hii, Ye alizungumza na Bloomberg na kueleza kwamba ni muda sasa wa yeye kufanya biashara peke yake. Alisema hakuna kampuni tena ambayo itasimama katikati yake na watu wake (wateja).


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii