Dully Sykes "Wasanii Wengine Wananiita Mjinga"

Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva princedullysykes ameamua kuvunja ukimya kufuatia baadhi ya wasanii wenzake wa zamani kumuona yeye kama mjinga anavyokuwa anafanya kazi na wasanii wa kizazi kipya.


Dully ambaye kwa nyakati tofauti ameonekana akifanya kazi na wasanii kama Kusah, Young Lunya na wengine, ameeleza hayo kupitia insta story yake, akiwaambia wenzake kuwa, kufanya kazi na wasanii hao sio kwamba ni kujishusha au ndio uwezo wao umeisha.


Watambue kwamba kuna muda wanapaswa wakubali kila kitu kina wakati wake, hivyo waishi kutokana na kizazi kinavyobadilika. Ameeleza dully


Pia ameendelea kueleza kwamba hawa wasanii wa leo walijifunza kutoka kwao, na wao ni wakubwa zao, hivyo waishi nao tu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii