OMMY DIMPOZ AMLIPUA BABA YAKE

Msanii wa bongo fleva , omary nyembo alimaarufu ommy dimpozi amesema baba yake mzazi alimtelekeza akiwa mdogo na hakuwahi kumuonesha mapenzi tangu azaliwe mpaka sasa.

akizungumza kupitia kipande cha video alichokiweka kupitia ukurasa wake wa instagram, dimpozi amesema anaitumia siku yake ya kuzaliwa  kwa kutoa ujumbe kwa wazazi watarajiwa.

"wazazi tunatakiwa kuwaonesha upendo watoto wetu hata kama hatuna kitu, mimi baba yangu hakunionesha mapenzi tokea utotoni, alinitelekeza lakini sasa hivi anaibuka na kusema anataka ajulikane kama yeye ndie baba mzazi wangu."

huu ujumbe kwetu mimi nilikua mtoto wa nje ya ndoa nafahamu  kabisa kuwa siwezi kurithi na yeye hawezi kurithi kwangu, hata hivyo nitakula na wale niliyohangaika nao, lakini sina tatizo nae ila sina mapenzi nae. amesema dimpoz

 HII NI VIDEO YA OMMY ZIMPOZ AKIZUNGUMAZA

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii