Umoja wa Mataifa wataka ushirikiano dhidi ya madhila ya ulimwengu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa mshikamano na ushirikiano ili kushughulikia ulimwengu ulio hatarini wakati wa ufunguzi wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa.

Akitolea mfano madhila ya migogoro na mabadiliko ya tabia nchi, mfumo wa kifedha uliovurugika duniani, katika hotuba yake hiyo Guterres amesema ulimwengu unakabiliwa na hali ngumu katika kudumisha amani, haki za binaadamu na maendeleo endelevu. zaidi alisema "Kushughulikia changamoto za pamoja kutahitaji mshikamano endelevu wakati tukionyesha ahadi kubwa na uwezo wa shirika hili. Umoja wa Mataifa ndio makao ya ushirikiano. Na Baraza Kuu ndio maisha ndani ya makao hayo.

Juma lijalo idadi kubwa ya wakuu wa nchi na serikali watapata kuzungumza katika hadhara kuu hiyo, pamoja na kwamba hadi sasa hakuna mabadiliko ya ratiba, mazishi ya Malkia Elizabeth II Jumatatu ijayo, ambayo idadi kubwa ya viongozi wanatarajiwa kuhudhuria, yanaacha maswali kuhusu ratiba ya shughuli za juma lijalo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii