Benki ya Dunia"Umaskini uliokithiri utaendelea kuwepo"

Benki ya Dunia imesema sio rahisi ulimwengu kulifikia lengo lake la kuondoa umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030.

Hayo yameelezwa katika ripoti mpya ya Benki ya Dunia iliyotolewa jana. Ripoti hiyo iliyopewa jina ''Umaskini na Ustawi wa Pamoja'' inaelezea maendeleo katika juhudi za kimataifa za kumaliza umaskini uliokithiri.

Ripoti hiyo imelitaja janga la virusi vya corona kama kizuizi kikubwa katika juhudi za kupunguza umaskini duniani kwa miongo kadhaa. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mwaka 2020 ulishuhudia zaidi ya watu milioni 71 wakiishi kwa dola 2.15 kwa siku au chini ya hapo.

Wachumi wa benki hiyo wamesema hali imekuwa mbaya zaidi baada ya Urusi kuivamia Ukraine, pamoja na kusuasua kwa uchumi wa China, mfumuko wa bei na kuongezeka kwa bei ya chakula na nishati. Hatua hizo zinaendelea kukwamisha maendeleo katika siku zijazo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii