Trump aishitaki CNN

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amelishtaki shirika la utangazaji la Marekani CNN kwa kumkashifu, akitaka kulipwa fidia ya dola milioni 75.

Trump ameishutumu CNN kwa kuendesha kampeni aliyoiita ya kashfa dhidi yake. Amedai kwamba kituo hicho kinataka kuvuruga juhudi zozote alizonazo za kisiasa za siku za usoni.

Amedai kwamba CNN ilitumia maneno “uwongo mkubwa” yenye maudhui ya Kinazi kwa zaidi ya mara 7,700 dhidi yake. Rais huyo wa zamani wa Marekani hata hivyo bado hajatamka wazi iwapo ana mipango ya kuwania tena urais katika uchaguzi wa 2024 baada ya kushindwa kwenye uchaguzi uliopita dhidi ya rais wa sasa Joe Biden.

CNN yenyewe haijasema chochote kuhusu kesi hiyo iliyowasilishwa na Trump katika mahakama ya Fort Lauderdale, Florida.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii