Picha za mvulana mdogo Mkenya aliyevalia mavazi ya polisi, akiwa na bunduki bandia pamoja na pingu za plastiki, zimevuma sana mitandaoni Mvulana huyo aliyeonekana akielekeza trafiki kwenye mitaa ya Nairobi akiwa na maafisa wa polisi, aliwashangaza wengi Wakenya wengi walisema picha hizo zinachekesha huku wengine wakidai kwamba, huenda ikawa ni sehemu ya masomo kwenye mtaala wa CBC nchini humo.