Timu ya Taifa ya Watu wenye ulemavu Tembo Warriors, imepata ushindi wa kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yanayoendelea nchini Uturuki wakiifunga Uzbekistan mabao 2-0
Ushindi huo mbele ya wababe wa kundi E umewafanya washike nafasi ya pili wakiwa na jumla ya alama nne ndani ya michezo mitatu waliyocheza huku miwili ya mwanzo wakivuna alama moja baada ya kupata sare ya bila kufungana na Hispania na wakifungwa mabao 3-0 na Poland.
Mabao mawili ya ushindi ya Tembo Warriors yamefungwa na Steven Manumbu dakika ya 13 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Alfan Kiyanga ambaye na yeye kipindi cha pili mnamo dakika ya 38 alipiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja ndani ya wavu licha ya kipa wa Uzbekistan kufanya jitihada za kutaka kuokoa mpira huo.