Uchaguzi kufanyika Oktoba 30 Brazil

Maafisa wa tume ya uchaguzi nchini Brazil wamesema kuwa duru ya pili ya uchaguzi itafanyika Oktoba 30, baada ya wagombea wawili wakuu kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazohitajika.

Baraza la Juu la Uchaguzi, TSE limesema huku asilimia 99.6 ya kura za uchaguzi wa jana zikiwa zimehesabiwa hadi sasa, Rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva mwanasiasa wa mrengo wa kushoto ameongoza baada ya kupata asilimia 48.3 ya kura halali, ikilinganishwa na Rais aliyeko madarakani Jair Bolsonaro kutoka chama cha mrengo wa kulia aliyepata asilimia 43.3.

Wagombea wengine tisa walikuwa wanashindana, lakini uungwaji mkono wao haulingani na wa Bolsonaro na da Silva. Utafiti wa maoni ya wapiga kura uliochapishwa Jumamosi na taasisi ya Datafolha ulionesha kuwa Lula atashinda kwa asilimia 50 dhidi ya Bolsonaro aliyetabiriwa kupata asilimia 36 ya kura.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii