Mlipuko mkubwa wa gesi uliotokea leo kwenye mfumo wa majitaka katika mji wa Shershah kusini mwa Pakistan umewauwa watu wasiopungua 12 na kujeruhiwa wengine 11.
Msemaji wa polisi ya mji huo Sohail Jokhio amesema mlipuko umetokea baada ya kitu kisichofahamika kuzusha moto na kusababisha gesi iliyolundika kwenye mfumo wa maji taka chini ya jengo moja la benki kulipuka.
Picha za video zilizopatikana na kurushwa na vyombo vya habari nchini Pakistani zinaonesha jengo la benki hiyo ya HBL limeharibiwa pamoja na magari yaliyoegeshwa karibu eneo kulikotokea mkasa huo.
Duru kutoka hospitali moja mjini humo zinasema miongoni mwa waliojeruhiwa, watatu wako kwenye hali mahututi. Polisi imesema tayari timu ya wataalmu imetumwa kwenda eneo la tukio kubaini chanzo cha moto uliochochea mlipuko