Damiba awataka waliofanya mapinduzi ''kuwa na fikra pevu''

Waandamanaji wenye hasira wameshambulia ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou jioni ya Jumamosi.

Hii ni baada wa wafuasi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi mapya kuituhumu Ufaransa kumpa hifadhi rais wa mpito aliyeangushwa Paul-Henri Sandaogo Damiba. Msemaji wa serikali ya Ufaransa Anne-Claire Legendre amesema wanalaani kwa nguvu zote ghasia zinazoelekezwa kwenye ubalozi wao, na kuongeza kuwa ''Kitengo cha dharura kimeundwa mjini Ouagadougou.

Umoja wa Afrika, AU pamoja na jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS vimekosoa vikali hatua ya wanajeshi wa Burkina Faso kuiangusha serikali. Huku Marekani ikisema inafuatilia kwa wasiwasi mkubwa yanayojiri nchini humo. Kupitia taarifa iliyochapishwa kupitia ukurasa wa Facebook Damiba amewataka wapinzani wake "kurejea katika hali ya umakini".

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii