Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ashawishi vikwazo dhidi ya Iran baada ya kifo cha Amini

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema anafanya kila lililo chini ya uwezo wake ili kufanikisha vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya wale wanaowakandamiza wanawake nchini Iran, wiki mbili baada ya kifo cha mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 22 nchini humo Mahsa Amini aliyekuwa chini ya kizuizi cha polisi wa kulinda maadili.

Baerbock leo ameliambia Bunge la Ujerumani kwamba mamlaka za Iran lazima zimalize mara moja ukandamizaji dhidi ya waandamanaji na kutoa wito wa uchunguzi kuhusu vifo vya Mahsa Amini na wale wanaoandamana kuhusiana na kifo chake.

Maafisa nchini Iran wanasema watu 41 wakiwemo maafisa wa polisi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wamepoteza maisha katika maandamano hayo kote nchini humo lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yameripoti idadi ya juu zaidi ya vifo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii