Sababu za kifo cha Malkia Elizabeth II za wekwa wazi

Chanzo cha kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza, ambaye alitawala kwa muda mrefu zaidi ya malkia au mfalme mwingine yeyeote wa nchi hiyo, kimetolewa rasmi.

Kulingana na cheti cha kifo kilichochapishwa Alhamisi na Rekodi za Kitaifa za Scotland, Elizabeth alikufa Septemba 8 kutokana na "umri mkubwa."

Wakati rasmi wa kifo uliorodheshwa kuwa saa tisa na dakika kumi alasiri.

Malkia Elizabeth, 96, alikuwa katika Kasri la Balmoral huko Ballater, Scotland, wakati wa kifo chake.

Kiongozi huyo wa kifalme alikuwa akipambana na matatizo ya mara kwa mara ya kiafya katika miezi ya mwisho ya maisha yake, hali ambayo mara nyingi ilimfanya kutumia fimbo kutembea, na mara nying kutojitokeza hadharani kama ilivyokuwa hulka yake katika miaka ya nyuma.

Mazishi ya Elizabeth yalifanyika tarehe 19 mwezi Septemba 2022.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii