Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema hakuna haja ya kuweka vikwazo ikiwemo marufuku ya kutoka nje katika maeneo yenye mlipuko wa Ebola kwasababu Ugonjwa huo hausambazwi kwa njia ya Hewa.
Hapo awali, Chama cha Wahudumu wa Afya kilitoa wito kwa eneo lililoathiriwa kuwekwa Karantini ili kukomesha kuenea zaidi kwa Maambukizi ambapo Museveni amesema Serikali yake ina uwezo wa kudhibiti janga hilo bila hatua hizo kuchukuliwa.
Pia, amesema Wataalamu wa Afya ambao hapo awali walishughulikia milipuko ya Ebola wametumwa katika eneo lililoathiriwa.