Magaidi wauawa na wanyama wakali.

Majeshi ya Msumbuji yamesema kwamba yamewakamata watu wanne ambao wanatokea vikosi vya kijihad nchini humo ambao wamekua wakiwakamata na kuwaua watu huku  vikosi hivyo vikitangaza kuwaua wengine 16. 


Kamanda wa polisi Bernardino Rafael amesema kwamba baadhi ya magaidi waliuawa kwa majeraha ya risasi wakati wakijibizana risasi na askari, huku wengine wakishambuliwa na wanyama wakali haswa Simba na Mamba .

Kamanda huyo alikua akitoa taarifa hiyo wakati akizungumza na wakazi wa wilaya ya  Quissanga iliyopo jimbo la  Cabo Delgado

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii