Urusi kuitisha kikao ha Baraza la Usalama

Urusi inapanga kuitisha mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili uharibifu uliofanywa katika mabomba hayo mawili. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova amesema hayo katika taarifa aliyoichapisha kwenye mtandao wa Telegram.

Serikali ya Urusi imekanusha tuhuma kwamba inahusika na uvujaji wa gesi katika mabomba hayo. Msemaji wa rais wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov amesema "ni ujinga na upuuzi kuwa na mawazo kama hayo".

Peskov amesema ni muhimu kusubiri uchunguzi katika maeneo yanayovuja na kubainisha kama uharibifu huo ulisababishwa na mlipuko ama la. Peskov pia amesema si kwa maslahi ya Urusi kwa gesi inayopitia kwenye mabomba hayo kuhujumiwa akisema gesi inasukumwa kwenye njia zote za bomba la Nord Stream 2.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii