Idadi ya watu waliofari dunia kutokana na ugonjwa wa ebola nchini Ugenda imefikia watu 21 huku zaidi ya 30 wakiwa wameambukuzwa.
Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Afya nchini Uganda imesema kuwa kuwa wizara inaendelea kufuatilia watu ambao wanaweza kuwa wamepata maambukizi ya ugonjwa huo.
Serikali nchini Uganda ilitangaza mlipuko wa ugonjwa wa ebola nchini humo Septemba 20 mwaka huu baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika katika Wilaya ya Mubende iliyopo katikati ya nchi hiyo.
Ebola ni ugonjwa wa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90. Shirika la afya duniani, (WHO) linasema kwa mara ya kwanza ugonjwa huo ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na nchini Sudan.