Tanzania Kuuza Tumbaku Japan Sasa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, wakati walipokutana kwenye kasri la Kifalme ambalo hutumika kufanyia shughuli za Kiserikali la Asaka (Asaka Palace), jijini Tokyo, Japan, Septemba 26.2022.


Kampuni ya Japan Tobacco Incorporation (JTI) imeahidi kununua kilo milioni 30 za tumbaku kutoka kwa wakulima wa Tanzania katika msimu ujao wa kilimo.

Ahadi hiyo imetolewa na Rais na Mtendaji Mkuu wa JTI, Bw. Masamichi Terabatake mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyetembelea ofisi zao ili kuwahakikishia utekelezaji wa mazungumzo yaliyofanyika wakati wa mkutano wa TICAD 8, jijini Tunis, Agosti, mwaka huu.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amesema uamuzi wa kampuni hiyo kuongeza kiwango cha ununuzi wa tumbaku utatoa ahueni kwa wakulima wa Tanzania ambao walikuwa hawana uhakika wa soko la zao hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii