Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kuacha kulalamika kuhusu kulegalega kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na badala yake itoe suluhisho kwa kuharakisha muswada wa bima ya afya kwa wote Bungeni, wakitaja ndiyo mwarobaini wa tatizo hilo.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipobainisha dalili za kufa kwa mfuko huo kutokana na kuelemewa na madeni ya matibabu ya wanachama wake huku akiyataja magonjwa sugu kuwa chanzo.
Aidha, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ya mashirika ya umma ya Machi 2022 inaonyesha NHIF ilipata hasara ya Sh109.71 bilioni.
NHIF pia inaidai Serikali kiasi cha Sh30.4 bilioni pamoja na mkopo usio na mkataba wa kiasi cha Sh129.04 bilioni, fedha ambazo zilichukuliwa na Serikali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, kwa mujibu wa ripoti ya CAG.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Stanslaus Nyongo alisema kwa hali ilivyo kama mfuko utabaki ulivyo utakufa na kwamba kamati hiyo imekuwa ikitoa mapendekezo yake mara kwa mara nini kifanyike kwa wizara ya afya.
“Serikali haitakiwi kulalamika, ije na suluhisho, tulishasema kwenye kamati mwarobaini wake ni kuwa na bima kwa watu wote maana yake tukiwa na bima ya aina hiyo mfuko utaimarika kifedha, watakaotoa fedha ni watu wazima hawaumwi hivyo utakuwa na nguvu,” alisema.