Mmoja wa vijana madaktari waliojiunga kwenye kikundi akizungumzia mradi wa zahanati walioijenga baada ya kupatiwa mkopo wa Sh110 milioni uliotokana na mapato ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kati ya vijana hao nane, wapo madaktari wawili, mfamasia mmoja, wataalam wa maabara wawili, wauguzi wawili na mwanasheria mmoja ambapo wameanzisha mradi huo kwenye eneo la Kipunguni kwa Mkolemba.