Wamiliki Wa Mabasi Ya Shule Yasiyokaguliwa Wakamatwa.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Georgina Matagi amewaweka mahabusu wamilikiwa wa shule tatu zilizoko Mjini Babati, kwa kushidwa kupeleka magari ya kubebea wanafunzi ili yafanyiwe ukaguzi na polisi.

Matagi amechukua uamuzi huo Agosti 31 baada ya wamiliki hao kushidwa kitii agizo la kupeleka magari ya shule zao kufanyiwa ukaguzi kabla ya shule kufunguliwa Septemba 5 2022 ili kubaini magari ambayo ni mabovu.

"Lengo letu ni kuhakikisha magari yanayobeba wanafunzi yanakaguliwa kwani kikubwa ni usalama wa watoto na magari yenyewe pia tumepata funzo kwa ajali iliyotokea Mtwara," amesema Matagi.

Hata hivyo, katika ukaguzi huo amebaini baadhi ya magari hayafai kutumika kutokana na ubovu na akachukua namba za magari hayo ili yaweze kufanyiwa matengenezo ndipo yabebe wanafunzi pindi shule zikifunguliwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii