Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, ndugu Nassib Bakari Mmbaga, kuanzia leo tarehe 30.08.2022 ili kupisha uchunguzi.
Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo sambamba na utendaji kazi usioridhisha.
Waziri Bashungwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu.