Rais Samia amefungua kikao kazi maafisa waandamizi Jeshi la Polisi

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania(TPS) mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ufunguzi kikao kazi cha Maofisa wakuu waandamizi wa polisi wa makao makuu, makamanda wa polisi wa mikoa na vikosi.

Kikao hicho ambacho ni cha siku tatu kinaanza leo Agosti 30 hadi Septemba Mosi, 2022 ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la polisi kila mwaka kufanya kikao kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji katika kipindi cha mwaka mmoja.

Katika kikao hicho wataangalia walipofanya vizuri na wapi ambapo hawakufanya vizuri na sababu zake ili kuweka mikakati mipya ya kutekeleza majukumu ya jeshi hilo kwa ufanisi zaidi katika mwaka unaofuata.

Katika kikao hicho viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Camillus Wambura, Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, Jacobo Mkunda pamoja na viongozi wengine wa serikali na viongozi wa dini.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii