Takwimu makosa ya jinai yaongezeka

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Camillus Wambura amesema takwimu za makosa makubwa ya jinai nchini zimeongezeka kipindi cha Januari hadi Juni mwaka 2022.

Amesema yameongezeka kutoka makosa 24,848 kipindi kama hicho mwaka 2021 hadi makosa 27,848 sawa na ongezeko la asilimia 11.2.

IGP Wambura ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 30,2022 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maofisa wa waandamizi wa Jeshi la Polisi makao makuu na makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi.

"Ongezeko hili linatokana na Jeshi la Polisi kufanya operesheni na misako mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu hali iliyopelekea ongezo la makosa hayo," amesema IGP Wambura.

Amesema miongoni mwao makosa hayo ni watu kupatikana na mirungi, bangi, pombe haramu ya moshi, watu kukutwa na nyara za serikali, mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi, ushirikina, ulevi na migogoro ya ardhi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii