NASA yaahirisha uzinduzi wa roketi kuelekea mwezini

Shirika la anga za juu la Marekani NASA limeahirisha uzinduzi wa roketi lenye nguvu uliopangwa kufanyika jana kutokana na tatizo la kwenye injini. Uzinduzi huo ni sehemu ya programu ya anga iliyopewa jina la Artemis ambayo inalenga kuwasafirisha tena binadamu kuelekea mwezini. Uzinduzi huo ulitarajiwa kufanyika kutokea kituo cha anga cha Kennedy jimboni Florida nchini Marekani. Endapo uzinduzi wake utafanikiwa, chombo hicho kitauzunguka Mwezi ili kuona ikiwa ni salama kwa watu katika siku za usoni. Ikiwa misheni mbili za kwanza za Artemis zitafanikiwa, NASA inalenga kuwasafirisha tena wanaanga mwezini mapema mwaka 2025, akiwemo mwanamke wa kwanza. Safari yake inatarajiwa kutumia siku 42 na kuzunguka mwezi kufikia ndani ya maili 60. Mara ya mwisho wanaanga kufika mwezini ni miaka 50 iliyopita, kupitia ujumbe wa Apollo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii