Majaji watano kutoka mataifa ya kigeni wamefika nchini kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya urais itakayoanza leo saa tano katika Mahakama ya Upeo.
Majaji hao wanachama wa Chama cha Majaji wa Afrika (AJJF), walitua nchini jana wakiongozwa na Jaji Mkuu (mstaafu) Mohammed Chande Othman wa Tanzania.
Majaji wengine katika ujumbe huo ni Lillian Tibatemwa-Ekirikubinza wa Mahakama ya Upeo Uganda, Ivy Kamanga wa Mahakama ya ya Upeo Malawi, Moses Chinhengo wa Mahakama ya Rufaa Lesotho na Henry Boissie Mbha ambaye ni Rais wa Mahakama ya Masuala ya Uchaguzi Afrika Kusini.