Venezuela na Colombia warudisha mahusiano kamili ya kidplomasia

Colombia na Venezuela wamerudisha tena mahusiano kamili ya kidplomasia, miaka mitatu baada ya Venezuela kukata uhusiano huo kufuatia hatua ya Colombia kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guaido. Balozi wa Colombia Armando Benedetti hapo jana aliwasili Mji Mkuu wa Venezuela Caracas huku balozi wa Venezuela Felix Plasencia akipokelewa katika Mji Mkuu wa Colombia Bogota hiyo hiyo jana. Katika ujumbe ulioandikwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, afisi ya rais wa Colombia imesema kwamba wameanza kujenga tena mahusiano yanayowaunganisha. Kabla kuondoka Benedetti alikuwa amesema kwamba lengo ni kujenga mahusiano na jirani yake na kurekebisha hasara waliyopata raia wa nchi hizo iliyotokana na kuharibika kwa mahusiano, jambo ambalo halikustahili kufanyika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii